
WEMA Isaac Sepetu amelidokeza gazeti alipendalo la Ijumaa Wikienda kuwa  ameitwa ikulu ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza kwa mwaliko. Wema alisema mwaliko huo aliupata mara tu baada ya kuzindua ile filamu yake ya  Super Star wiki mbili zilizopita ambapo katika mwaliko huo wa ujumbe kutoka  ikulu hiyo ulimuomba kutoisambaza kwanza kabla ya kwenda kuizindua nchini  humo.
“Waliniambia juu ya mimi kuomba uraia wa nchi hiyo ili kukuza filamu  zao. Kusema kweli nilikuwa nina ratiba ya kwenda kuizindua filamu yangu Rwanda,  Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Yaani sijui hata walijuaje. Sijui  ni nini kimetokea, nina wasiwasi. Hata sijui nitaongea nini na Rais wa Burundi,”  alisema Wema na kuongeza kuwa maandalizi yakikamilika atatii wito huo muda  wowote.
source: kilinyepesi blog
Monday, 9 July 2012
WEMA AITWA IKULU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment